Ufunuo 17:8
Print
Mnyama unayemwona alikuwa hai kwanza, lakini sasa si hai. Hata hivyo, atapanda kutoka kuzimu na kwenda kuangamizwa. Watu wanaoishi duniani watashangaa watakapomwona mnyama, kwa sababu aliwahi kuwa hai, hayuko hai, lakini atakuwa hai tena. Hawa ni watu ambao majina yao hayajawahi kuandikwa katika kitabu cha uzima tangu mwanzo wa ulimwengu.
Huyo mnyama uliyemwona alikuwapo lakini sasa hayupo , naye atapanda kutoka katika shimo la kuzimu kwenda maangamizoni. Na watu waishio duniani ambao majina yao hayakuandikwa kwenye kitabu cha uzima tangu ulimwengu kuumbwa, watashangaa kumwona huyo mnyama, kwa maana alikuwapo, na hayupo, na kwamba atakuwapo.
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU) Copyright © 2017 by Bible League International; Neno: Bibilia Takatifu (SNT) Copyright © 1989 by Biblica